Phellipe Coutinho alifunga bao lake la 17 nje ya Box tangu ajiunge na Liverpool na hivyo kumfanya kuwa mchezaji wa Epl mwenye mabao mengi zaidi nje ya box.
Hiyo ilikuwa katika suluhu ya leo kati ya Liverpool ambao walikuwa ugenini kukipiga dhidi ya Newcastle United huku bao la Newcastle likifungwa na Joselu.
Katika mchezo mwingine Nacho Monreal alifunga bao lake la kwanza tangia March 2013, Iwobi naye akifunga bao lake la kwanza Epl tangu January 31 wakati Arsenal wakiiua Brighton bao 2 kwa 0.
Nchini Hispania hii leo matukio ya kisiasa yalichukua sehemu kubwa lakini hayakuzuia Lioneil Messi kukaa kilele cha ufungaji baada ya kupiga mabao mawili dhidi ya Las Palmas.
Sergio Bosquets alifunga bao lingine la 3 hili likiwa bao lake la kwanza kuifungia Barcelona ndani ya miaka mitatu na kuwafanya Barcelona kuibuka kidede kwa ushindi wa mabao 3 kwa 0.
Post a Comment