0
Tume ya mawasiliano nchini Uganda (UCC) imepiga marufuku vyombo vya habari nchini humo kufanya mahojiano na Mbunge wa upindani Bobi Wine, baada ya kuonekana kinara kwenye suala la kupinga ukomo wa urais nchini humo.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Bobi Wine ambaye pia ni mwanamuziki nchini humo  ameandika kuwa amepigiwa simu na baadhi ya vyombo vya habari nchini humo na kuthibitisha suala hilo, kuwa wamepigwa marufuku kufanya naye mahojiano yoyote.
“Hii asubuhi nilitakiwa kufanya mahojiano na Capital FM, baadaye nikataarifiwa kuwa wamepewa agizo na UCC na kupigiwa simu na watu wa usalama kwamba wasiwe na mimi, nikapigiwa simu na vituo vingine vya redio na runinga na kunithibitishia wamepewa agizo hilo hilo na kwa vitisho, na iwapo watakuwa na mimi watakuwa katika hatari ya kufungiwa”, ameandika Bobi Wine.
Bobi WIne amekuwa miongoni mwa viongozi maarufu ambao wanapinga vikali suala la kutaka kupitishwa kwa katiba ambayo itongeza muda wa ukomo wa urais, kitendo ambacho kitamruhusu Rais Yoweri Museveni wa nchi hiyo, kugombea tena awamu ijayo.

Post a Comment

 
Top