0


Pichani Balozi Asha Rose Migiro akipokea Fulana hiyo.


Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Dkt. Asha - Rose Migiro leo aliandaa hafla fupi katika makazi ya Balozi kumpongeza kijana mtanzania Alphonse Simbu alieshika nafasi ya tano katika mbio za "London Marathon" zilizofanyika tarehe 23 Aprili 2017 jijini London.
Katika salamu zake, Balozi Migiro alimpongeza Bw. Simbu kwa heshima aliyoipa Tanzania jijini London na Duniani  kupitia mbio za London. alimsihi atumie matokeo hayo kama hamasa ya  kufanya bidii zaidi kwa ajili ya mashindano ya mbio ndefu anayotarajiwa kushiriki baadae mwakani.
Simbu alimshukuru Balozi Migiro Kwa ushirikiano mkubwa wa kibalozi alioupata akiwa jijini London.Alimkabidhi Balozi Fulana ya kumbukumbu ya ushiriki wake kwenye mbio hizo.

Post a Comment

 
Top