Katika
harakati za kurudisha kwa jamii kile anachokipata, mkali wa wimbo
‘Marry You’, Diamond Platnumz, ameweka wazi mpango wake wa kujenga
hospitali ya moyo na magonjwa mengine katika mtaa aliozaliwa, Tandale
Jijini Dar es salaam.
Muimbaji alisema tayari amefanya mazungumzo na wadau mbalimbali na wamemuahidi kumpatia vifaa kwa ajili ya hospitali hiyo.
Akiongea
na waandishi wa habari Ijumaa hii wakati akizindua perfume yake mpya
‘CHIBU’, Diamond alisema hospitali hiyo itawasaidia Watanzania wa hali ya
chini.
“Mafanikio
yote tunayopata hatusahau kurudisha kwa jamii kile tunachokipata,”
alisema Diamond. “Ukiachana na misikiti ambayo nimekuwa nikiijenga
katika mikoa mbalimbali nchini Tanzania habari nje kwa ndugu zangu wa
Tandale ni kwamba nataka kuwajengea hospitali ambayo itakuwa inatoa
huduma pale kwa bei nafuu,”
Aliongeza,
“Kuna wadau wangu wanakaa nje, nimezungumza nao wameniambia nijenge tu
nay wao kuna baadhi ya vifaa wataleta. Kwa hiyo nikaona hii ni fursa na
tayari kuna baadhi ya mambo ya mwanzo tumeanza kuyashughulikia. Nataka
ufike muda watu waache kwenda kusafiri nje kutibiwa magonjwa mbalimbali
kama moyo na mengine ambayo yamekuwa akitufanya tusafiri nje kwa ajili
ya matibabu,”
Perfume aliyozindua muimbaji huyo imeanza kuuzwa rasmi leo nchini kwa bei ya Tsh. 105000.
Post a Comment