0
Baada ya Chelsea kutangulia fainali za FA zitakazopigwa tarehe 27 mwezi ujao kwa kuitoa Tottenham sasa timu hiyo inaenda kukutana na Arsenal katika mchezo wa fainali.
Arsenal wameingia katika fainali hizo baada ya kuitoa Man City kwa jumla ya bao mbili kwa moja katika mchezo ambao ulilazimika kuongezwa dakika 30 baada ya zile 90 za mwanzo kuisha kwa suluhu ya moja kwa moja.
Katika mchezo huo alianza kufunga Kun Aguero baada ya kumhadaa golikipa wa Arsenal dakika ya 62 na kufunga bao la kwanza kabla ya Nacho Monreal kuisawazishia Arsenal dakika kumi baadae.
Mpaka dakika 90 zinaisha matokeo ilikuwa bao ni moja kwa moja ndipo muamuzi aliamua kuongeza dakika 30, dakika ya 101 mabeki wa Man City walijichanganya na kumfanya Alexis Sanchez kutumia makosa yao kuipatia Arsenal bao la pili.
Baada ya mchezo huo kuisha hivyo sasa ina maana Arsenal wanakwenda Wembley kuikabili Chelsea katika fainali itakayopigwa May 27, na hii inaweza kuwa imewapa matumaini mapya Arsenal haswa katika kipindi hiki ambacho waliandamwa na matokeo mabovu.

Post a Comment

 
Top