0
Mwanasoka bora wa dunia Cristiano Ronaldo ana rekodi nyingi,lakini ana mambo mengine ambayo ni nadra kuyafahamu, hivi umeshawahi kujua haya kuhusu yeye?

1. Cristiano Ronaldo ni jina moja. Tofauti na watu wengi wanavyojua kwamba Cristiano na Ronaldo ni majina tofauti lakini kiuhalisia jina lake la kwanza ni Cristiano Ronaldo kisha ndio linafuatia “Dos Santos Aveiro”, jina hili la Ronaldo alipewa kutokana na wazazi wake kuvutiwa na raisi wa Marekani Ronald Reigan.

2. Alishawahi kutaka kuachana na soka. Alipokuwa na miaka 15 Cristiano Ronaldo alipata matatizo ya moyo, moyo wake ulikuwa ukimuenda moyo kila akikimbia na hii ilimfanya atakr kuachana na soka lakini baada ya operesheni alipona na kuendelea na soka.

3. Ni mwanafunzi asiye na nidhamu. Maisha ya Ronaldo ya shule hayakuwa mazuri hata kidogo kwani alikuwa mkorofi kupitiliza, alipokuwa mdogo alipata matatizo shuleni baada ya kumrushia mwalimu wake kiti.

4. Alitazamwa na watu wengi zaidi siku anatua Madrid. Kabla ya Ronaldo kwenda Madrid, Diego Maradona alikuwa akishikilia rekodi ya kuwa mchezaji aliyejaza sana watu uwanjani wakati akitambulishwa alitazamwa na mashabiki 74,000 lakini wakati Ronaldo anatambulishwa Real Madrid watu zaidi ya 79,000 walihudhuria.

5. Anamkubali sana Arnold. Kama ulikuwa hulijui hili nikuambie tu kwamba Cristiano Ronaldo ni shabiki wa kutubwa wa mwigizaji Arnold Shwarzenigar,na amekuwa akifuafilia sana movir zake pia akivutiwa na umbo lake

Post a Comment

 
Top