Kukiwa
na wasiwasi kwamba Korea Kaskazini inakaribia kupata ufanisi wa
kukamilisha silaha za Kinyuklia, Marekani imepewa onyo la kutoanzisha
uchokozi dhidi ya nchi hiyo kwani ipo tayari kulipiza kisasi kwa
mshambulio ya Kinyuklia.
”Tuko tayari kulipiza kisasi na mashambulio ya Nyuklia kwa mbinu zetu dhidi ya shambulio lolote la Kinyuklia”.
Taarifa
hiyo imetolewa wakati Rais wa nchi hiyo, Kim Jong-un alipohudhuria
gwaride la heshima katika mji mkuu wa Pyong yang katika maadhimisho ya
siku ya kuzaliwa ya babu yake, marehemu Kim II-Sung, ambaye ni
mwanzilishi wa taifa hilo.
Mtu
ammoja anayedaiwa kuwa na uwezo mkubwa katika nchi hiyo amesema kuwa
wamejiandaa kwa vita kamili. “tumejiandaa kwa vita kamili” amesema
Aidha,
katika gwaride lililofanyika, vifaa vilivyoonyeshwa kwa mara ya kwanza
vilikuwa ni makombora ya masafa marefu yanayoweza kwenda kwa takriban
kilomita 1000 na nyingina nzito ambapo wachanganuzi wa vifaa vya kijeshi
pia wamesema kuwa kuna makombora mawili mapya yanayoweza kurushwa
kutoka bara moja hadi jingine, lakini haijulikani iwapo yamefanyiwa
majaribio.
Post a Comment