Rais
Magufuli leo wakati akizindua majengo ya Hostel za Chuo Kikuu Cha Dar
es Salaam (UDSM) amefunguka na kusema sasa anasubiri ripoti ya
wafanyakazi wa Serikali zaidi ya elfu tisa ambao wanatumia vyeti vya
kufoji.
Rais
Magufuli amesema kumekuwa na changamoto kubwa katika kila sekta hivyo
sasa anasubiri hiyo ripoti ili aweze kuifanyika kazi na kutenda haki
katika jambo hilo.
"Naisubiri ripoti ya wafanyakazi wa Serikali zaidi ya elfu tisa ambao wana vyeti vya kufoji ili niifanyie kazi" alisema Rais Magufuli
Mbali
na hilo Rais Magufuli ameitaka Taasisi ya TCU kuacha kuwapangia
wanafunzi vyuo bali wanafunzi wanapaswa kuwa huru kuchagua aina ya vyuo
ambavyo wao wanataka kwenda na kusema kwa kufanya hivyo itatoa nafasi
kila chuo kuwa na wanafunzi wa kutosha huku wanafunzi pia wakienda
kusoma sehemu ambazo wao wanahitaji kwenda kusoma na si kuwapangia.
"Mtu
amefaulu ana sifa zake anataka kuja kusoma Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam
afaidi mabweni ya Magufuli analazimishwa kupelekwa kwenye ka chuo
ambako wala hakana jina hata ukitafuta kwenye mtandao hakaonekani,
akasome pale wakati hawana hata mabweni na saa zingine hata walimu
hawana, tunawatesa watoto hawa na saa zingine wakuu wa vyo vile wamekuwa
na tabia ya kwenda kwenye uongozi wa TCU ingawa sina ushahidi wapangiwe
idadi wa wanafunzi wanaowataka kwenye vyuo hivyo, sifahamu wanapangiwa
kwa rushwa lakini wapo pia kuna ushahidi na baadhi ya viongozi wa vyuo
fulani fulani waliofunga safari kwenda TCU kwa ajili ya kuomba wapangiwe
wanafunzi au kutoa shukrani, au hata kwenda kuwasalimu tu" alisema Rais Magufuli
Post a Comment