0
 
 
Mshukiwa mmoja aliyekuwa anasakwa kwa kuhusika na mashambulio ya mabomu katika makanisa nchini Misri katika miji ya Tanta na Alexandria amejisalimisha kwa polisi, Shirika la utangazaji nchini humo Mena limeripoti.

Mdokezi kutoka idara ya usalama alisema kuwa mshukiwa huyo aliyetambuliwa kama Mohamed Ali Hassan, alipelekwa kwenye makao makuu ya shirika la usalama wa kitaifa.

Kiongozi wa Wakristo wa Coptic, Papa Tawadros II, alikuwemo katika kanisa moja kati ya mawili yaliyolengwa Jumapili ya Matawi mwanzoni wa mwezi huu, ambapo watu 45 waliuwawa katika mashambulio hayo ambayo yalidaiwa na kundi la Islamic State.

Mashambulio dhidi ya Wakristo, ambao huwa takriban asilimia 10 ya idadi ya watu nchini Misri, ilizua hali ya hofu mbele ya kuzuru kwa Papa Francis mjini Cairo, ambaye ni kiongozi wa kanisa la Katoliki , inayotarajiwa kati ya 28-29 Aprili.

Post a Comment

 
Top