0
 
 
Chameleone amekanusha tetesi kwamba mkewe Daniella Atim amekwenda mahakamani kudai talaka.

Taarifa zilisambaa mitandaoni kwamba Daniella alidai kwa kutokuwa na furaha na ndoa yake kutokana na manyanyaso na vipigo anayoyapata kutoka kwa muimbaji huyo mkongwe wa Uganda.

Chameleone ameamua kuvunja ukimya kupitia mtandao wa Facebook kwa kurusha video ya dakika 53 akiongelea mengi kuhusu familia yake, ambayo inaonekana kuwa na furaha tofauti na yanayozungumzwa.

“Kuna habari nyingi zimesambaa zinazohusu mimi na familia yangu. Siwezi kusema kubwa lolote lakini nachotaka kusema ni kuwa sina talaka wa hakuna anayedai talaka,” amesema msanii huyo kwenye video hiyo.

“The beautiful Daniella there. Kumbuka mimi ni mkatoliki, mkatoliki akifunga ndoa hawezi kuachana,” ameongeza

Post a Comment

 
Top