Rais
wa Tanzania Dkt. John Magufuli amepokea barua yenye ujumbe wa Rais wa
Jamhuri wa Rwanda Mhe. Paul Kagame iliyowasilishwa kwake na Mjumbe
Maalum ambaye ni Waziri wa Elimu wa Rwanda Dkt. Musafiri Papias Malimba.
Pamoja
na kupokea barua hiyo, Mhe. Rais Magufuli na Dkt. Musafiri Papias
Malimba wamezungumzia masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania
na Rwanda ikiwemo katika sekta ya elimu hususani maendeleo ya sayansi
na teknolojia.
Aidha,
Mhe. Rais Magufuli ameipongeza Rwanda kwa kuamua lugha ya Kiswahili
ianze kufundishwa katika shule zake na ameahidi kuwa Tanzania ipo tayari
kutoa walimu wa kwenda kufundisha lugha hiyo.
Post a Comment