Msanii wa nyimbo za injili Tanzania Flora ambaye alikuwa mke wa Emmanuel
Mbasha jana amefanikiwa kufunga ndoa yake ya pili na kijana Daudi
Kusekwa baada ya ile ya kwanza kuvunjika na kupeana talaka na Emmanuel
Mbasha.
Baaada ya kufunga ndoa hiyo jana Flora alisema yeye ana amani ya moyo
licha ya watu kuendelea kusema maneno juu yake na maisha yake.
Flora amesema yeye hajali jinsi gani watu wanamtazama kutokana na
maamuzi yake hayo bali yeye anachoangalia ni furaha yake na kusema kwa
sasa yeye ana amani na furaha ya moyoni na hayo maisha mapya, ambayo
ameamua kuwa nayo.
"Unapofanya maamuzi na kuhisi kwamba unaamani na uko sawa sawa just do
it, kwa sababu wanadamu tumeubwa kusema hata huyo ambaye umekaa naye
karibu hapo anaweza kuonyesha kukufurahia, hata mtu ambayo yupo karibu
na wewe anaweza kuwa anakuchekea ukajua kama ni rafiki yako kumbe ni
adui yako mkubwa, kwa hiyo unapokuwa unataka kufanya jambo na kuhisi una
amani ya moyo bora ufanye maana wanadamu hawachoki kuzungumza" alisema
Flora
Flora Henry jana jijini Mwanza alifunga ndoa yake ya pili na kijana
anayefahamika kwa jina la Daudi Kusekwa ambaye ni mwenyeji wa jiji la
Mwanza na baada ya ndoa hiyo Mume wa Flora, Daudi Kusekwa alifunguka na
kuwataka Watanzania sasa watambue kuwa Flora si mke wa mtu mwingine bali
ni mke wake yeye halali
Post a Comment