Msanii mkongwe anayetamba kwa sasa na wimbo wa 'Unanimaliza', Rehema
Chalamila ' Ray C' amefunguka kuwa machozi huwa yanamdondoka pindi
anapomsikilizisha mtu wimbo ambao anaamini utafanya vizuri alafu
akajibiwa hautokuwa 'hit'.
Ray C amefunguka hayo leo kwenye Planet Bongo wakati akitambulisha wimbo
wake mpya na kueleza kuwa kabla hajapeleka wimbo kwenye Radio huwa
anasikilizisha watu na anapopata majibu tofauti na alivyofikiria huwa
yanamuumiza na kumfanya atengeneze ngoma nyingine kali akiwa na
machozi.
"Kabla sijatoa wimbo nina tabia ya kuwasikilizisha watu wa chache ambao
naamini wana sikio la muziki. Huwa sichukii nikiambiwa wimbo ni mbaya
lakini machozi huwa yananitoka kwa sababu mimi naamini nimetengeneza hit
alafu mtu anakwambia hamna kitu. Hata huu wimbo wa unanimaliza ndio
ulipita kati ya nyimbo tano nilizotengeneza na nyingine zilizobaki
wamenishauri nisiziweke kwenye albam"- Ray C alifunguka.
Aidha Ray C amewataka wasanii wengine kutojiamini kupitiliza kiasi cha
kuchukua wimbo studio na kuupeleka kwa mashabiki pasipokupata ushauri
kwani kufanya hivyo ndicho chanzo cha nyimbo kupoteza ladha mapema.
Post a Comment