0
Image result for uti symptoms
Ugonjwa wa (U.T.I) ni miongoni mwa magonjwa ambayo yamekuwa yakiwasumbua wasichana wengi sana, nenda mashuleni huko utastajabu ya Musa, kwani ugonjwa huu umekuwa ni kero kwa wanafunzi wengi sana. Lakini kwa elimu ndogo tuliyonayo wengi wetu hudhani ugonjwa huu huwapata mabinti peke yao, la hasha si kweli hata wanaume na wavulana huugua ugonjwa huu.
Ili kuweza kuepukana na magonjwa haya yanatokanayo mambukizi ya njia ya mkoja unashauriwa kutumia vyakula vifutavyo.

1. Nanasi
Kula Nanasi mara kwa mara ni mbinu nzuri kabisa katika kudhibiti maambukizi katika njia ya mkojo. Kwenye nanasi kuna kimeng’enya mhimu sana kijulikanacho kwa kitaalamu kama ‘Bromelain’
Katika utafiti mmoja, watu wenye U.T.I waliopewa hii bromelain sambamba na antibiotic zao walifanikiwa kuondokewa na maambukizi ya U.T.I.
Kula vipande vitatu mpaka vitano vya nanasi kila siku kutakuweka mbali na ugonjwa huu.

2. Kunywa maji safi na salama kila wakati.
Kama unasumbuliwa na U.T.I au inakutokea unapatwa na ugonjwa huu mara kwa mara, basi hakikisha unakunywa maji ya kutosha kila siku walau glasi 8 mpaka 10 kwa siku, maji yenye joto la kawaida yaani yale ambayo hayana ubaridi.
Mara nyingi mtu mwenye U.T.I huwa ana upungufu wa maji mwilini na ikiwa utauchunguza mkojo wake utaona ni wa rangi ya njano.

Kunywa maji ya kutosha kila siku na kama matokeo yake bakteria wote wanaokupelekea upatwe na U.T.I watalazimishwa kutoka nje ya mwili kupitia mkojo utakaoupata kutokana na kukojoa mara kwa mara kama matokeo ya kunywa maji mengi na utaona baada ya siku 4 mpaka 7 hata rangi ya mkojo inabadilika na kuwa mweupe kabisa.

3. Kitunguu swaumu:
Kitunguu swaumu ni mojawapo ya tiba mbadala ya nguvu katika kutibu maambukizi kwenye njia ya mkojo. Ni dawa nzuri dhidi ya bakteria na virusi na hivyo moja kwa moja kuwa mhimu katika kutibu U.T.I ya jumla na hata ile ya kibofu cha mkojo.

Kwakuwa moja ya kazi ya kitunguu swaumu ni kusafisha mkojo basi ni dhahiri inafaa sana katika kutibu U.T.I. Namna ya kukitumia; Chukuwa kitunguu swaumu kimoja na ukigawe na uchukuwe punje 6, menya punje moja baada ya nyingine na kisha kikatekate (chop) vipande vidogo vidogo na kisu kisha meza kama unavyomeza dawa nyingine yoyote na maji vikombe 2 (nusu lita) kila unapoenda kulala kwa siku 7 hivi au zaidi.

4. Tumia Limau/ndimu:
Weka vijiko vikubwa vitatu vya juisi ya limau au ndimu ndani ya glasi moja ya maji (robo lita) na unywe yote. Fanya zoezi hili kutwa mara tatu.

Pia unaweza kuongeza asali vijiko vikubwa vitatu ndani yake. Mchanganyiko huu wa limau na maji ya uvuguvugu utakuondolea maumivu yatokanayo na U.T.I na hata kuzuia kutokwa na damu kama matokeo ya maambukizi ya U.T.I hasa kwenye kibofu cha mkojo.

Post a Comment

 
Top