0
Wakati David Trezeguet akimaliza maisha yake ndani ya klabu ya Juventus alikuwa amefunga mabao 32, toka kipindi hicho hadi usiku wa jana hakuna mchezaji wa Juve ameshawahi kufunga mabao 30 lakini goli la kwanza la Higuain dhidi ya Monaco limempa idadi hiyo ya mabao.
Higuain almanusra afanye kile alichofanya Cristiano Ronaldo katika mchezo wao dhidi ya Atletico kwa kufunga hattrick, kwani Higuan tena katika dakika ya 59 aliipatia Juventus bao la pili kabla ya kocha wake kumtoa na nafasi yake kuchukuliwa na Juan Cuardrado.

Mchezo huo ulikuwa ni wa 63 kwa Higuain toka aanze kushiriki michuno ya Champions League lakini hii ilikuwa mara yake ya pili kufunga mabao mawili kwenye mchezo mmoja katika mashindano hayo makubwa barani Ulaya.
Katika mchezo huo safu ya ushambuliaji ya Monaco ilicheza vizuri na katika kipindi cha kwanza Kylian Mbappe na Radamel Falcao walionekana wakiichachafya beki ya Juventus lakini uimara wa beki ya Juve na kipa wao uliwanyima bao Monaco.

Matokeo hayo yanawafanya Monaco kuwa na mlima mrefu wiki ijayo watakaposafiri kwa mechi ya marudiano, inaonekana ni ngumu sana kuwafunga Juventus lakini Monaco watapaswa kugangamala na kuwafunga Juve mabao matatu ili kuweza kufudhu kwa fainali ya michuano hiyo msimu huu.

Kabla ya mchezo huo mchambuzi nguli wa masuala ya soka Shaffih Dauda aliitabiria Juventus kutinga fainali ya michuano hiyo ya Ulaya na kubeba kombe,na sasa utabiri huo umeanza kuonekana kama unaenda kutimia kwa Juventus kuichungulia fainali itakayopigwa tarehe 3 mwezi ujao mjini Cardiff.

Post a Comment

 
Top