Georgina Rodriguez ni jina maarufu sana nchini Hispania na duniani, mlimbwende huyu alipata umaarufu baada ya kuanza kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanasoka bora wa dunia Crstiano Ronaldo.
Baada ya habari kwamba Georgina Rodriguez ana ujauzito wa Ronaldo ndipo ambapo karibu kila mmoja alitaka kumjua Georgina na huku kukiwa na taarifa ya kwamba wawili hao wanaelekea kufunga ndoa.
Pamoja na furaha yote inayoendelea ndani ya mapenzi ya Georgina na Cr7 lakini nyuma ya pazia kumejificha story ambayo inamkosesha raha mlimbwende huyo na ingekuwa Afrika tungesema ndoa yao iko mashakani.
Georgina ametengwa na wazazi wake, baba yake aitwaye Jorge Eduardo na mama yake aitwaye Anna Maria hawako katika mahusiano mzuri na binti huyo na inadaiwa hata hawajali kuhusu ujauzito wa binti huyo.
Hii inamfanya Georgina kubaki mpweke kwani baba yake aliyeko Argentina na mama yake aliyeko Italia wameshindwa kwenda kumjulia hali jambo linalomuumiza mlimbwende huyo na kumfanga Ronaldo awe mtu pekee wa faraja kwake.
Ronaldo na Georgina wanatarijia kupata mtoto wa nne ambaye ni wakike katika familia yao, huku tayari wakiwa na Cristiano Jr na wiki kadhaa zilizopita waliwakaribisha Eva Mari na Matteo ambao ni mapacha.
Post a Comment