Shirika la afya duniani WHO limetangaza kuwa zaidi ya masaa 14.6 milioni yanapotezwa kila siku kwa ulaji wa mirungi huko Yemen.
Ulaji wa mirungi ulianzia Ethiopia,ukaenea hadi nchi za Afrika Mashariki,Yemen, Zimbabwe, Zambia, Malawi na hata Afrika kusini.
Mirungi ilionekana kuwa ni moja ya madawa ya kulevya hivyo ikakatangazwa na umoja wa mataifa UN na kupigwa marufuku mwaka 1971 kwasababu ya ufanano wa kemikali iitwayo amphetamine.
Yapo madhara mengi ya kiuchumi, kidini nk. Lakini yafuatayo ni madhara ya kiafya ya mirungi kama ilivyofanywa na shirika la afya duniani kama ifuatavyo;
MADHARA YA KIAFYA;
- Mtumiaji wa mirungi yupo katika hatari ya kupata vidonda vya tumbo.
- Kupungukiwa msukumo wa kufanya tendo la ndoa (low sex drive) na
- pia kuwahi kumaliza haraka na kutoweza kudumu kwenye tendo la ndoa kwa muda mrefu
- Ukosefu wa haja kubwa (constipation)
- Utumiaji wa muda mrefu husababisha ini kushindwa kufanya kazi,pia meno kubadilika rangi, kudhoofika,fizi kuuma na harufu mbaya mdomoni
- Upungufu wa usingizi
- Humpelekea mlaji kutawaliwa nayo(addiction)
- Madhara ambayo bado kinamama walaji Mirungi hawajagundua ni kwamba mtoto anayezaliwa na mama mlaji Mirungi mara nyingi hukataa kunyonya titi la mama yake kwa sababu ladha ya maziwa inabadilika kwa ajili ya utumiaji wa madawa (pesticides) unaotumiwa na wakulima wa Mirungikama inavyoeleza utafiti uliofanyika na Chuo Kikuu Cha Aden (Aden University).
- Utafiti mwengine kule Ethiopia unatueleza ya kuwa mtoto wa mama mwenye kula Mirungi kwa wingi huwa hana uzito wa kawaida wakati wa kuzaliwa.
- Ukosefu wa hamu ya kula chakula
Post a Comment