Hali ya kisiasa nchini Hispania sio nzuri hata kidogo, siku ya jana kulitokea machafuko na polisi kuwaladhimu kutumia nguvu za ziada kuwatawanya raia wa Catalunya ambao wanadai uhuru wao.
Jana mchezo wa Las Palmas dhidi ya Barcelona almanusra usichezwe baada ya Barcelona kutaka kugomea mchezo huo kuonesha kuungana kwao na raia wenzao wa Catalunya wanaodai uhuru.
Inasemekana jaribio la Barcelona kutotaka mchezo huo upigwe liligongwa mwamba baada ya shirisho la soka Hispania kuwatisha na adhabu kubwa ikiweml kuwafungia kucheza ligi kwa muda wa miezi 6.
Barcelona waliingia uwanjani kupambana na wakaibuka na ushindi wa bao 3 kwa 0 na kuendelea kujikita kileleni lakini kitendo cha Barcelona kukubali kucheza mchezo huo kimeleta madhara kwenye klabu.
Makamu wa raisi wa klabu hiyo Carles Villarubi ni mmoja kati ya waliojiuzulu hapo jana huku mkurugenzi Jordi Mones naye akibwaga manyanga, bado raisi wa Barcelona Maria Bartomeu anasubiriwa kutoa tamko kuhusu tukio la jana.
Post a Comment