Biashara ya kubet imekuwa ikishika kasi barani Afrika kila siku huku makampuni mengi yakianzishwa na kujikusanyia watu wanaopenda kufanya hivyo.
Leo May 2, 2017 good news kwa watu wangu wanaopenda michezo ya kubahatisha ‘betting’ kwamba wasikate tamaa kwa sababu upo uwezekano mkubwa wa kushinda kama ambavyo Mkenya huyu ameshinda.
Mtandao maarufu wa BBC umeripoti kuwa Samuel Abisai, 28, kutoka Kenya ameshinda Dollar 2m (£1.6m) zaidi ya Tsh. 4.5b
baada ya kushinda utabiri wa mechi 17 za kandanda na kumfanya kuwa mtu
wa kwanza kushinda kiasi hicho cha fedha kupitia betting kwenye historia
ya soka la Afrika.
Samuel ameshinda kiasi hiko cha fedha baada ya kutumia Dollar 2 kwa machaguo mawili tofauti, kwa mujibu wa SportPesa ambapo kutokana
na ushindi wa fedha hizo, Abisai anapanga kutoa sehemu ya ushindi huo
kwa jamii yake, ikiwa ni pamoja na kuisaidia klabu yake ya mtaani mkoa
wa Magharibi wa Kakamega.
Post a Comment