Wamerakani weusi wengi wamekuwa hawapendi sera za raisi mpya wa nchi hiyo Donald Trump, mmoja kati ya watu ambao wameonesha wazi hisia zao kuhusu Trump ni mfalme wa basketbaal Steph Curry.
Curry aliweka wazi wazi kwamba hata siku moja hawezi kukanyaga ikulu ya White House kama akialikwa na raisi Donald Trump kwani anataka kuionesha dunia hisia zake juu ya utendaji kazi wa raisi huyo.
Curry amesema kukataa kwake kwenda ikulu kutaleta mabadiliko chanya kwa raisi na wananchi ambapo watajua wazi kwamba raisi hayuko katika njia sahihi na hivyo yeye Curry yuko upande wa wasiokubaliana na raisi.
“Sitaki kwenda, naamini hii itaonesha ni jinsi gani hatusimamii upande wa yale anayoyaamini, mambo ambayo amesema siyaungi mkono na naamini jambo hili ninafanya litasaidia kufikisha ujumbe kuhusu yeye” alisema Curry.
Baada ya Curry kukataa mualiko wa Donald Trump raisi huyo alienda moja kwa moja kwenye ukurasa wake wa Twitter na kuandika kwamba kama Curry amekataa kwenda baasi mualiko umefutwa.
Trump hakuishia hapo bali alisema kumuita kwake Curry na Golden State Warriors ilikuwa ni heshima kubwa kwao kufika mahala hapo, na kusisitiza kwamba ili ufanikiwe zaidi katika michezo lazima uwe na heshima.
Wananchi mbalimbali nchini Marekani wamekisifu kitendo cha Curry na kumuona kama mmoja wa watu ambao yuko upande wao na huku wakimuona kama shujaa mpya.
Le Bron James ni mmoja kati ya watu ambao wamesema wazi kwamba Curry amefanya kitu sahihi sana na kusisitiza kwamba hakuna haha ya mualiko kama watu hawataki kwenda. Toka Trump aingie madarakani amekuwa akikosolewa sana na raia wake kuhusu sera za utawala wake.
Post a Comment